Utoaji elimu ya bima: TIRA yashiriki maadhimisho miaka 30 ya VETA

Machi 20, 2025 Dar es Salaam
Katika kuunga mkono shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo cha Ufundi Stadi Tanzania (VETA), TIRA inashiriki maonesho yaliyoandaliwa na chuo hicho kutoa elimu ya bima kwa umma ambayo yanafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam kuanzia tarehe 18 - 21 machi 2025.
VETA inaadhimisha miaka thelathini (30) tangu kuanzishwa kwake ambapo maadhimisho hayo yameambatana na maonesho ya huduma na bidhaa kutoka taasisi za serikali na yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Kassim Majaliwa tarehe 18 machi 2025 na ameipongeza VETA kwa tukio hilo muhimu linalotoa picha kujadili mafanikio, changamoto na mikakati yake.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA) inashiriki maonesho hayo kwa siku zote nne lengo likiwa kutoa elimu ya bima kwa kuwaelimisha wananchi majukumu yake, umuhimu wa kutumia bidhaa za bima za kawaida na za maisha lakini pia kueleza fursa zilizopo katika sekta ya bima nchini.
Wananchi wote mnakaribishwa pia unaweza kutembelea tovuti yetu tira@go.tz kwa habari na matukio yanayoendelea katika sekta ya bima.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA