Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Unganisheni nguvu kukinga majanga ya Afrika.
02 Dec, 2022
Unganisheni nguvu kukinga majanga ya Afrika.

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amezitaka kampuni za bima barani Afrika kuunganisha nguvu ili kutoa kinga dhidi ya majanga ya kiuchumi na kijamii.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Mamlaka za usimaizi wa bima barani Africa iliyofanyika jijini Arusha.

“Nashauri wataalum wa bima muone umuhimu wa kuunganisha nguvu zenu kwa pamoja ili kuepusha upelekaji wa fedha za bima nje ya nchi pasipokuwepo na ulazima, kumbukeni Umoja ni nguvu” alisema Mhe. Majaliwa.

Pia, amewataka kushirikiana kutoa kinga kwa majanga mbalimbali kwenye shughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi na afya ambako majanga na athari yanaongezeka kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

 Mhe. Majaliwa amezitaka kampuni za bima barani Afrika kuendelea kutoa elimu ili kuchochea uelewa wa matumizi ya bima barani Afrika.

       

“Takwimu kuhusu uelewa wa bima barani Afrika zinaonyesha kwamba bado tuko nyuma sana na tunahitaji kuongeza juhudi na kuweka mikakati ya pamoja ili jamii ielewe umuhimu wa bima na kutumia huduma za bima kwa ajili ya maendeleo yao” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware amesema soko la bima nchini liko tayari kupokea wawekezaji katika maeneo ya kilimo, uvuvi na shughuli za bima mtawanyo.

Mkutano huu umewaleta pamoja wasimamizi wote wa sekta ya bima barani Afrika kwa ajili ya kujadili changamoto zinazokabili sekta ya bima barani Afrika.