Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA yakutana na wadau wa Zanzibar, yajadili uboreshaji wa huduma
22 Feb, 2025
TIRA yakutana na wadau wa Zanzibar, yajadili uboreshaji wa huduma

TIRA YAKUTANA NA WADAU WA BIMA ZANZIBAR, YAJADILI UBORESHAJI WA HUDUMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imekutana na wadau wa sekta ya bima katika mkutano maalum wa kupokea maoni na mapendekezo ya kuboresha huduma za bima nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idris Abdulwakil, Kikwajuni, Zanzibar.  

Katika hotuba yake kabla ya kuanza kwa majadiliano, Naibu Kamishna wa TIRA, Khadija Issa Said, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisisitiza kuwa bima ni nyenzo muhimu inayotoa kinga dhidi ya majanga, hivyo ni lazima kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu umuhimu wake.  

Aliwataka wadau wa sekta ya bima kuongeza uwazi na uadilifu, hasa katika kushughulikia madai ya wateja, ili kujenga imani ya wananchi kwa sekta hiyo. Pia, aliwasihi kampuni za bima kuhakikisha wanalipa fidia kwa wakati na kwa haki.  

Katika hadhara hiyo washiriki walitoa maoni kuhusu changamoto wanazokutana nazo huku wakisisitiza juu ya kupatiwa elimu kuhusu maswala ya bima ili kuweza kutatua changamoto hizo zikiwemo namna ya kufuatilia madai
Katika Mkutano huo watoa huduma za bima mbalimbali walikuwepo kujibu hoja za wateja ambao ni Kampuni za bima za Bumaco, Icealion, Shirika la bima la Zanzibar, Milembe, Heritage, CRDB, Tanzindia, Jubilee na kadhalika lakini pia alikuwepo mwakilishi wa  Kampuni ya bima Mtawanyo ya Grandree.