Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA na wadau washiriki utoaji elimu kwa umma; maadhimisho Wiki ya Huduma za Fedha Tanga
25 Jan, 2026
TIRA na wadau washiriki utoaji elimu kwa umma; maadhimisho Wiki ya Huduma za Fedha Tanga

Ushirika wa Mamlaka na kampuni za bima umejidhihirisha wazi katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea mkoani Tanga, ambapo elimu ya bima imetolewa kwa wananchi waliojitokeza na kuelimishwa kuhusu bima, leo Januari 25, 2026 katika viwanja vya usagara.

Akizungumza katika darasa hilo; Afisa Takwimu Bima kutoka TIRA Bw. Ayubu Mremi alieleza dhamira ya Mamlaka katika utekelezaji wa bima ya afya kwa wote na vifurushi pendekezwa ambavyo vitawawezesha wananchi kupata huduma za bima ya afya kulingana na kipato.

Pia, kampuni za bima zilizoshiriki zilipata nafasi ya kufafanua bidhaa za bima wanazotoa kwa wananchi na kampuni hizo ni pamoja na Britam Insurance, Meticulous Insurance, Sanlam Allianz na kampuni ya bima mtawanyo ya Grand Re.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA