Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Tira yaanzisha kanda ya Kusini.
18 May, 2023
Tira yaanzisha kanda ya Kusini.

Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware ametembele Ofisi za Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ili kutambulisha Ofisi za Mamlaka Kanda ya Kusini. 

Katika ziara hiyo Dkt. Saqware alipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Zuwena Omary Jiri na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lini. SAC. E. Kabaleki.

Dkt. Saqware alibainisha kuwa uamzi wa Mamlaka kufungua ofisi hizo ni kuhakikisha huduma za usimamizi wa bima zinasogezwa karibu na wananchi na kuhakikisha soko la bima linawafikia wananchi wengi.

Akizungumzia uwepo wa Mamlaka katika Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena aliipongeza Mamlaka kwa uamuzi huo kwani mkoa wa Lindi ni katikati ya mikoa ya Mtwara na Ruvuma jambo ambalo litarahisisha wananchi kupata huduma.

Pia, Kamanda Kabaleki alisema Jeshi la Polisi liko tayari kushiriakiana na watendaji wa Mamlaka anda ya Kusini ili kuhakikisha sheria ya bima inatekelezwa. 

Mamlaka imefungua Ofisi za Kanda ya Kusini Mkoani Lindi ambayo itahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.