Zoezi la Ukaguzi wa Bima za vyombo vya moto lashika kasi Shinyanga na Kahama
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Magharibi inaendelea kuratibu na kusimamia zoezi la ukaguzi wa bima za vyombo vya moto katika mkoa ya Shinyanga na Kahama, ambapo limefanyika kwa mkoa wa Shinyanga Januari 5 – 6, 2026 na linaendelea leo Januari 7 – 9, 2026 Kahama; ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wamiliki wa vyombo hivyo wanazingatia matakwa ya kisheria ya kuwa na bima halali.
Zoezi hilo linafanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ambapo akizungumzia umuhimu wa Bima kwa vyombo vya Moto, Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ACP Zainab Mangala amesema bima hizo ni jambo la lazima na ni msaada mkubwa yanapotokea majanga na kuwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakata bima.
Kwa upande mwingine, Meneja wa TIRA Kanda ya Magharibi Bi. Awanje Matenda amesisitiza kuwa wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakata na kutumia bima halali kutoka kwa kampuni zilizosajiliwa na pia amewarai wasafiri wote kuhakiki chombo cha moto kabla ya kukipanda, ili wajiridhishe iwapo kimekatiwa Bima kwa kutumia mfumo wa TIRAMIS katika simu ya mkononi, ambao unamuwezesha mtu yeyote kufanya utambuzi.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA
