Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda awahimiza wananchi kutumia huduma na bidhaa za bima

Leo machi 20 2025, Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda ametoa rai kwa watanzania kutumia huduma na bidhaa za bima na kutosubiri hadi pale majanga yanapotokea. Mhe. Pinda ameyasema hayo alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika maadhimisho ya miaka 30 ya VETA yanayofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam yaliyoanza tarehe 18 machi hadi 21 machi 2025.
Aidha Waziri Mkuu huyo mstaafu alisisitiza elimu ya bima itolewe zaidi kwa wananchi wa mjini na vijijini ili kuongeza idadi ya wanaofahamu kuhusu bima na hatimaye kutumia na kuhamasisha wengine ili kuweza kulinda afya, mali na uwekezaji.
Kwa siku ya tatu sasa TIRA inashiriki maadhimisho hayo kwa kutoa elimu na kusikiliza maoni mbalimbali yanayotolewa na wananchi wanaotembelea banda lao. TIRA imekuwa ikishirikiana na VETA katika mambo mbalimbali ya utoaji elimu na uhamasishaji wa matumizi ya bima nchini.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA