Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Watumishi wa TIRA Wapatiwa Mafunzo Kuhusu Afya ya Akili, Magonjwa Sugu na Maadili ya Utumishi wa Umma
31 Dec, 2025
Watumishi wa TIRA Wapatiwa Mafunzo Kuhusu Afya ya Akili, Magonjwa Sugu na Maadili ya Utumishi wa Umma

Leo tarehe 31 Desemba, 2025 jijini Dar es Salaam, watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) wamepatiwa mafunzo maalum yaliyojikita katika masuala ya afya ya akili, magonjwa sugu pamoja na maadili ya Utumishi wa Umma. Mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi kazini sambamba na kuhamasisha umuhimu wa kuzingatia afya ya mwili na akili ili kutekeleza majukumu ya kazi kwa viwango vinavyotakiwa.

Kupitia mafunzo hayo, watumishi walielimishwa kuhusu namna ya kujikinga na vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao, kuzingatia maadili na misingi ya Utumishi wa Umma, pamoja na umuhimu wa kuishi maisha yenye uwiano kati ya kazi na maisha ya kawaida (work-life balance) kwa ajili ya ustawi binafsi na wa taasisi kwa ujumla.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA