Viongozi TIRA watembelea ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini
27 Sep, 2025

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Bima (CPA. Moremi Marwa) na Kamishna wa Bima (Dkt. Baghayo Saqware) leo Jumamosi tarehe 27 Septemba 2025 wametembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini ikiwa ni mualiko wa Mhe. Balozi Togolani Mavura katika jitihada za kuhakikisha Tanzania inapata Ujuzi na Uzoefu wa Usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA