Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Uzinduzi wa Akaunti ya dhamana ya benki ya Watu wa Zanzibar
04 Dec, 2023
Uzinduzi wa Akaunti ya dhamana ya benki ya Watu wa Zanzibar

Leo tarehe 04/Desemba 2023, Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, wamezindua Rasmi Akaunti ya dhamana ya benki ya Watu wa Zanzibar. Akitoa hotuba yake ya Ufunguzi wa Semina hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlangila uliopo Hotel ya Peacock Jijini Dar es salaam, Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo A. Saqware alieleza lengo   kuu la akaunti ya dhamana ni kukinga fidia endapo Kampuni ya Bima itafilisika au kupata hasara. Lakini pia akaunti ya dhamana italeta uaminifu kwa wateja wa Bima na itawafanya wajiamini kwa kukata Bima. Hivyo akaunti ya dhamana ipo kwa ajili ya kulinda haki ya wateja wa Bima.