TIRA yazindua Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa Mwaka 2024; mafanikio, changamoto na mikakati sekta ya bima yatajwa

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezindua Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2024 ikilenga kuonyesha maendeleo, changamoto na mwelekeo wa sekta ya bima nchini. Uzinduzi huo umefanyika Octoba 17, 2025; TIRA Bima House jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya bima, wakiwemo watoa huduma, makampuni ya bima na wawakilishi wa Serikali ambapo ilielezwa Mchango wa Bima katika pato la taifa nchini umeongezeka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware, amesema sekta ya bima inaendelea kukua kwa kasi ambapo mchango wa Bima katika pato la taifa umeongezeka hadi kufikia 2.08% mwaka 2024 kulinganisha na 2.01%mwaka 2023, kwa upande wa Wakata bima na wanafaika wa bima kuna Ongezeko la 10.2%, Kutoka 23.5Mil hadi 25.9Mil sawa na asilimia 39.2 ukilinganisha na asilimia 37.7 mwaka 2023, ikimaanisha Wakatabima wam efikia 8.4Mil. na Wanufaikaji 17.5Mil.
Taarifa hiyo pia ina takwimu mbalimbali kuhusu Uendelezaji Soko la Bima, Masuala ya Usuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO), Madai ya Bima yaliyolipwa kwa kipindi husika, Watoa huduma waliofanya vizuri katika Soko ambao pia walitambuliwa na kupewa tuzo maalumu kutambua mchango wao.
Dkt. Saqware pia alieleza kuwepo kwa changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya bima ambapo Mamlaka imejipanga kwa Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Bima ambapo wananchi wengi watafikiwa na kuongeza ujumuishi katika sekta lakini pia maboresho ya huduma kwa njia za kidigitali yataongezeka kwa maendeleo ya Taasisi, sekta ya bima na wananchi kwa ujumla.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango Zanzibar, Mhe. Saada Mkuya Salum ambaye aliipongeza TIRA kwa mafanikio hayo na kusisitiza uendelevu wa ushirikiano kutoka kwa Serikali na Sekta ya bima kwa maendeleo ya umma. Taarifa hiyo inapatikana katika tovuti ya TIRA ambayo ni www.tira.go.tz.