Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA yatoa Semina ya Elimu ya Sheria ya Bima kwa Mahakimu jijini Dar es Salaam
12 Sep, 2025
TIRA yatoa Semina ya Elimu ya Sheria ya Bima kwa Mahakimu jijini Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) imeendesha semina ya elimu ya Sheria ya Bima kwa Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 12 Septemba.

Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa mpana kuhusu masuala ya bima na kuongeza ufanisi katika kushughulikia mashauri yanayohusiana na sekta hiyo. Kupitia semina hiyo, TIRA imelenga kuimarisha ushirikiano na mhimili wa mahakama ili kuhakikisha utekelezaji wa sheria za bima unafanyika kwa ufanisi, uwazi na kwa manufaa ya wananchi.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA