Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA yashiriki Mjadala kuhusu Usimamizi, Ubunifu na Ushirikiano katika Soko
26 Sep, 2025
TIRA yashiriki Mjadala kuhusu Usimamizi, Ubunifu na Ushirikiano katika Soko

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki katika Mkutano wa Umoja wa Madalali wa Bima (TIBA) unaondelea katika hoteli ya Golden Tulip visiwani Zanzibar ambapo leo Septemba 26, 2025 imeongoza Mjadala unaohusu Usimamizi (Regulation), Ubunifu (Innovation), na Ushirikiano (Collaboration) kwa lengo la kukuza sekta ya bima ili kuongeza ufanisi, utoaji huduma jumuishi na kulinda maslahi ya wananchi.

Wadau katika sekta waliohudhuria Mkutano huo walipata nafasi ya kujadili kwa kina kuhusu juhudi zinazofanywa na Mamlaka kutatua changamoto mbalimbali, ikiwemo athari za maendeleo ya teknolojia kama matumizi ya Akili Mnemba (AI).

Katika maelezo yake, TIRA ilisisitiza dhamira yake ya  kuhakikisha soko la bima linabaki salama kwa wadau na wateja kwa kuandaa mikutano ya mara kwa mara kama na wadau katika sekta ya bima wakiwemo TIBA ambapo kupitia mikutano hiyo na majukwaa tofauti shirikishi Mamlaka inapata sauti za wadau moja kwa moja na hatimae kupata maduluhisho ya maswala mbalimbali yenye kuzingatia hali halisi ya sekta.

Mamlaka pia ilieleza kuhusu maboresho ya mifumo ya kidijitali inayolenga kupunguza urasimu, kuongeza uwazi, na kurahisisha ufuatiliaji wa madai pamoja na huduma za bima kwa ujumla. 

Mjadala huo muhimu katika Sekta ya Bima ulishirikisha viongozi mbalimbali katika sekta wakiwemo Bi. Magreth Mngumi, Msuluhishi wa Migogoro ya Bima ambaye alimuwakilisha Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware, Bwn. Zakaria Muyengi, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Bwn Bahati Ogola Meneja wa Ukaguzi na Utekelezaji Sheria, Bwn. Ali Othman, Meneja wa TEHAMA na Mwendesha mjadala alikuwa Bi. Josephine Laswai kutoka UNDP.


Majadiliano hayo ni matokeo ya Mkutano wa siku mbili unaoendelea visiwani hapo ambapo ulifunguliwa rasmi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said