Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA YAFANYA UKAGUZI  WA  BIMA ZA VYOMBO VYA MOTO, ZAIDI YA MAGARI 450 YAKAGULIWA MANYARA
12 Sep, 2024
TIRA YAFANYA UKAGUZI  WA  BIMA ZA VYOMBO VYA MOTO, ZAIDI YA MAGARI 450 YAKAGULIWA MANYARA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia ofisi yake ya Kanda ya kati iliyopo  jijini Dodoma, imefanya ukaguzi wa vyombo vya moto katika eneo la Mererani wiłayani Simanjiro mkoani Manyara. 

Ukaguzi huo  ulianza  Septemba 9 na unatarajiwa kumalizika Septemba 12, 2024. Ambapo umelenga kukagua bima katika vyombo hivyo vya moto na kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia  bidhaa za bima. 

Hadi kufikia Septemba 11, magari zaidi ya mia 450 yamekaguliwa. Ukaguzi huu wa vyombo vya moto unafanywa kwa kushirikiana na wadau wengine kama Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama barabarani, EWURA, kampuni za bima na wakala wa bima. 

Pia vituo mbalimbali vya mafuta vitafanyiwa ukaguzi ili kuhakikisha sheria na kanuni za bima zinafuatwa. Na hii ni kutokana na sheria ya  Mafuta ya mwaka 2015 ambayo inavitaka vituo vyote vya mafuta kuwa na bima ya majanga. 

Faida  ya Bima ya vyombo vya moto ni pamoja na kumsaidia mtumiaji kujikinga na hasara pindi anapopata ajali na pia usalama pale anaposababisha ajali kwa mtu mwingine. TIRA Kanda ya Kati inahudumu mikoa ya Dodoma, Manyara na Iringa.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA