Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA YASHIRIKI MKUTANO WA WANAWAKE KWENYE SEKTA YA FEDHA
03 Apr, 2024
TIRA YASHIRIKI MKUTANO WA WANAWAKE KWENYE SEKTA YA FEDHA

Tarehe 14 Machi, 2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Waliopo Kwenye Sekta ya Fetha (TAWIFA) pamoja na Taasisi ya Mwanamke foundation (MIF)  wameadhimisha Siku ya Mwanamke duniani kwenye sekta ya fedha katika Ukumbi wa Kwanza Hotel uliopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. 

Maadhimisho hayo yaliambatana na Uzinduzi wa Chama cha Wanawake Waliopo kwenye Sekta ta Fedha ambapo Mgeni Rasmi wa shereke hizo alikuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
Wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa TAWIFA Dkt. Samia amewataka wanawake wajibiidishe katika kazi zao ili waweze kupata nafasi za juu katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya fedha. Aliendelea kwa kusema kuwa wanawake sasa tutoke kwenye harakati tuje kwenye utendaji au utekelezaji wa harakati hizo ili tusonge mbele katika maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla. 
Sherehe hizo zilihudhuriwa na wanawake wengi wakiwemo viongozi kama vile Mawaziri, Wake wa Marais  waliopita, wakuu wa Taasisi pamoja na viongozi wa chama na serikali.