Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA yashiriki Mkutano na Watendaji Wakuu wa Kampuni za Bima
13 Oct, 2023
TIRA yashiriki Mkutano na Watendaji Wakuu wa Kampuni za Bima

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware pamoja na Wakurugunzi wa Idara na Mameneja wa Kanda/Vitengo TIRA leo Octoba 13 , 2023 wamehudhuria Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Kampuni za Bima unaofanyika Kizimkazi Zanzibar.
Mkutano huo ulioandaliwa na TAN- RE na unaangangazia maswala mbalimbali yanayohusu kampuni hizo za bima na kuangalia namna bora ya kutatua changamoto kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa na TIRA kwakushirikiana na wadau wa bima.
Wakati akitoa wasilisho lake Kamishna wa Bima amesema ni wajibu wa kampuni za bima kutoa elimu kwa wakata bima wakati wanapoingia mikataba ya bima ili kuwapa uelewa juu ya stahiki zao wakati wa majanga lakini pia kujua wajibu wao kabla ya majanga.
Aidha Kamishna amezitaka  kampuni hizo kuelezea mafanikio yao katika ulipaji wa madai mbalimbali kwa wadai/wanufaika wa bima ili kuendelea kujenga Imani ya wananchi, watunga sera na serikali kwa ujumla dhidi ya watoa huduma za bima.