TIRA, NMB KUHAKIKISHA BIMA INAMFIKIA KILA MATANZANIA
12 Sep, 2025

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Septemba 11, 2025 imefanya kikao cha mashirikiano na wanahisa wa benki ya NMB kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na sekta ya bima nchini.
Kupitia kikao hicho, TIRA na NMB wamekubaliana kuweka mikakati endelevu itakayowezesha kila Mtanzania kufikiwa na huduma za bima kupitia mifumo na mitandao ya kibenki.
Aidha, pande hizo mbili zimejadili namna benki zinavyoweza kuchangia katika kukuza sekta ya bima nchini, hususan katika eneo la bima za kilimo, pamoja na kushirikiana katika utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.