Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA na Wiki ya Huduma kwa Wateja: Tunasimamia Msingi wa Maadili Yetu: Uweledi, Kumjali mteja, Umoja, Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi
08 Oct, 2025
TIRA na Wiki ya Huduma kwa Wateja: Tunasimamia Msingi wa Maadili Yetu: Uweledi, Kumjali mteja, Umoja, Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeungana na Taasisi mbalimbali nchini kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2025 kuhamasisha watumishi na wadau wote wa sekta ya bima kutambua umuhimu wa kutoa huduma bora, zenye ubora kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za TIRA katika kuimarisha uhusiano kati ya watoa huduma za bima na wateja wao.

Kupitia maadhimisho haya, TIRA imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma na misingi ya uwajibikaji. Mamlaka imekuwa ikisisitiza matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma, upatikanaji wa taarifa kwa uwazi, na kusikiliza maoni ya wananchi ili kuhakikisha huduma za bima zinabaki kuwa jumuishi, zenye kuaminika na zinazojibu mahitaji halisi ya jamii.

Si hivyo tu, kupitia kanda kumi za TIRA zilizopo Tanzania Bara na Visiwani TIRA imesogeza huduma za bima kwa wananchi ili waweze kujikinga na bima pamoja na mali zao. Lakini pia Mamlaka inatoa taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii mathalani kuhusu Sheria, Miongozo, Kanuni na Taratibu mbalimbali zinazoongoza soko la bima. Mitandao hiyo ni pamoja na Mtandao wa Kijamii wa Instagram tira_tz, Thread tira_tz, lakini pia na Tovuti ya Mamlaka www.tira.go.tz.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA