TIRA na wadau wakutana kujadili utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote Arusha
Tarehe 18 Desemba 2025, Mkoa wa Arusha umefanya kikao kazi maalum kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiwa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya. Kikao hicho kiliwakutanisha viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakurugenzi, RMO, DMOs, CMT, CHMTs, DED, Wakuu wa Vituo vya Afya, NHIF, Wizara ya Afya, RS, Viongozi wa Dini pamoja na wadau wa Bima ya Afya wakiwemo wahusika wote (in-charges) wa vituo vya afya vya serikali na binafsi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Arusha.
Lengo la kikao kazi hicho lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, mikakati yake pamoja na utoaji wa elimu ya Bima ya Afya. Washiriki wa kikao walipatiwa elimu kuhusu utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote na kuweka maazimio ya kueneza elimu hiyo kwa walengwa wakuu ambao ni wananchi.
Katika kikao hicho, Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Dkt. Lupilya, aliwasilisha wasilisho lililolenga kueleza namna ambavyo TIRA imejipanga katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, uwepo na umuhimu wa Mamlaka hiyo katika mfumo wa Bima ya Afya, pamoja na namna madai na migogoro itakavyoshughulikiwa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa katika sheria ya bima
