Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA na Konsotia ya bima ya kilimo washiriki Maonesho ya Nane Nane Dodoma; Elimu na uhamasishaji Bima za kilimo waelezwa
04 Aug, 2025
TIRA na Konsotia ya bima ya kilimo washiriki Maonesho ya Nane Nane Dodoma; Elimu na uhamasishaji Bima za kilimo waelezwa

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na Umoja wa Kampuni za bima zinazotoa bima ya kilimo (TAIC) zinashiriki Maonesho ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma katika viwanja  vya Nzuguni kuanzia tarehe 1- 8 Agosti 2025. Lengo likiwa kutoa elimu ya bima lakini pia kuhamasisha matumizi ya bima ya kilimo katika kilimo, ufugaji na uvuvi.

Aidha, wananchi mbalimbali mnakaribishwa katika mabanda ya Taasisi za Serikali banda namba moja kwa elimu na kupata maoni na taarifa mbalimbali za bima.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA