Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA NA JAMII, JAMII NA TIRA : BIMA NA MICHEZO, TIRA YATOA ZAWADI FAINALI POLISI JAMII CAP
08 Sep, 2024
TIRA NA JAMII, JAMII NA TIRA : BIMA NA MICHEZO, TIRA YATOA ZAWADI FAINALI POLISI JAMII CAP

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) jana Septemba 7, 2024 imejumuika pamoja na wananchi mbalimbali wa Ikwiriri wilayani Rufiji kuhitimisha mashindano ya Polisi Jamii Cup ngazi ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji. 

TIRA imedhamini mashindano hayo ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo polisi na kampuni za Bima. Kurudisha kwa Jamii (ufadhili ) hasa katika michezo, ni jambo ambalo Mamlaka ya Usimamizi wa Bima imekuwa ikifanya kwa  lengo la kuileta jamii karibu na kutoa elimu kuhusu bima.

Afisa Bima Ndg. Joseph Mfoi alihitimisha kwa kutoa elimu ya bima kwa  wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Mabatini lengo likiwa kila Mwananchi afahamu na kutumia Bidhaa za bima. Pia Mratibu Mkuu wa Polisi Jamii  Mkoa wa Kipolisi Rufiji,  ASP J. B Ibrahim aliishukuru Mamlaka kwa kuendeleza ushirikano Mara kwa mara.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ina jukumu la kutoa elimu ya bima, kulinda na kuendeleza soko la bima nchini, kusimamia kampuni za bima na hata kuishauri Serikali kuhusu masuala la bima nchini. Lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu kuhusu bima.