Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA kuondoa changamoto za kibima mkoani Tanga
01 Jan, 2026
TIRA kuondoa changamoto za kibima mkoani Tanga

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imedhamiria kuondoa changamoto mbalimbali kuhusu bima zinazowakabili Wananchi wa mkoa wa Tanga.
Hayo yameelezwa leo Desemba 31, na Meneja wa TIRA kanda ya kaskazini Dkt. Emmanuel C. Lupilya anayehudumia mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga wakati akitoa wasilisho lake kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC) kilichojadili hali ya maendeleo na changamoto zilizopo ili kuboresha huduma kwa wananchi wake.

Dkt. Lupilya ameendelea kueleza kuwa eneo ambalo linapewa kipaumbele ni usimamizi wa bima za afya na huduma zinazotolewa kwa wasajiliwa wote ili kuendana na matakwa ya sheria ya bima ya afya kwa wote hivyo Wananchi wote wanaaswa kujiunga kwenye mfumo huo wa Bima kwa mustakabali mzuri wa afya zao na wategemezi wao na kwamba TIRA itahakikisha changamoto zitakazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

TIRA kwa Soko salama la Bima