TIRA KANDA YA ZIWA TANGANYIKA YASHIRIKI MAADHIMISHO WIKI YA MWANAKATAVI
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Kanda ya Ziwa Tanganyika inashiriki kwenye maadhimisho ya Wiki ya Mwana Katavi katika viwanja vya Azimio wilayani Mpanda. Maadhimisho hayo yameanza rasmi Octoba 25 na yanatarajiwa kumalizika Octoba 31 2024.
Lengo kuu la ushiriki huu kwa Mamlaka ni kutoa elimu ya bima na kuwahimiza wananchi kutumia bidhaa za bima, lakini pia kuelimisha kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka zikiwemo kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima, kuandaa na kutoa kanuni na miongozo katika soko la bima, kulinda haki za mteja wa bima, lakini pia kuendeleza, kusimamia uhimilivu na uendelevu wa soko la bima.
Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko ambapo katika msimu huu wa Kilimo Mkuu wa Mkoa aliwahimiza wananchi kulima kwa kufuata mbinu bora na kuhakikisha wanajikinga na majanga kwa kutumia bima za kilimo.
Maafisa mbalimbali wameendelea kutoa elimu ya umuhimu wa Bima kwenye shughuli za kiuchumi kama Kilimo, Mifugo, Mazao na Biashara, ambayo inatolewa kwa wananchi na makundi mbalimbali na pia kupata huduma kutoka kwenye kampuni za bima. Pia elimu ya Bima kwa vyombo vya moto imetolewa na kuwahimiza wanachi kukagua vyombo vya usafiri wanavyotumia kwa kutumia mfumo wa TIRAMIS.
Wananchi wa Katavi wanakaribishwa katika Maonesho hayo ili wapate elimu ya bima na kufahamu fursa zilizopo katika soko la bima.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA