Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA ndani ya Tanzanite Trade Fair Manyara
19 Oct, 2023
TIRA ndani ya Tanzanite Trade Fair Manyara

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kupitia Kanda ya Kati inashiriki kwenye Maonesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair ambapo leo October 18, 2023 Mhe. Exaud Kigahe (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara anafungua rasmi maonesho haya.

Awali Dkt. Baghayo Saqware Kamishna wa Bima Tanzania Amemuleza Naibu Waziri alipotembelea banda la TIRA kuwa 
Sekta ya kilimo imeshaingia kwenye Bima kwani Konsotia ya kilimo imeanzishwa na kufikia mwezi Julai mwakani Bima za kilimo zitaanza kuingizwa Sokoni.

TIRA inashiriki maonesho haya ili kuendelea kutekeleza maagizo ya Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2020/2030 kutoa elimu kuhusu bima kwa wananchi na wafanyabiashara ili kuweza kuingia kwenye biashara ya bima kwakuwa wateja, wakala au washauri.

TIRA- Kwa soko salama la bima