Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Taarifa ya Soko la Bima kwa mwaka 2022 yazinduliwa Rasmi
08 Dec, 2023
Taarifa ya  Soko la Bima kwa mwaka 2022 yazinduliwa Rasmi

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania chini ya Kitengo cha Kurugenzi  ya Usimamizi wa Soko ikiongozwa na  Mkurugenzi  Abubakari Ndwata imezindua rasmi Taarifa ya Soko la Bima kwa mwaka 2022 katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 06 Desemba 2023. Wakati wa hotuba yake ya Taarifa ya Soko, Dkt. Baghayo A. Saqware, ambaye ndiye Kamishna wa Bima alieleza mafanikio yaliyofikiwa na Soko la Bima kuwa  ni makubwa sana ukilinganisha na miaka iliyopita. Mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa Kampuni za Bima kutoka 33 mpaka kufika Kampuni 40 zikiwemo na Bima Mtawanyo kuongezeka kwa Mawakala wa Bima, kuongezeka kwa Washauri wa Bima pamoja na Watakwimu Bima na kadhalika. Dkt. Saqware aliendelea kwa kusema kuwa,  Sekta hii ndogo ya Bima pia imechangia pato la Serikali kiasi cha aslilimia 1.68 kwa mwaka 2022.  Kamishna huyo alimalizia kwa kupongeza  Kampuni za Bima kwa kulipa  Fidia kwa Wahanga mbalimbali. Naye Mgeni Rasmi Dkt. Damas Ndumbalo, Mhe. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo aliipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kusimamia vema Soko la Bima na kuiingizia Serikali pato la Taifa. Akizindua taarifa hiyo, Dkt. Ndumbalo alizialika Kampuni za Bima kwende kuwakatia Bima wanamichezo kwa kuwa wanamichezo wapo kwenye hatari ya kuumia. Vile vile alisisitiza Kampuni za Bima zijitahidi kulinda haki za mteja wa bima na hasa kwa waliopo Vijijini.

Tukio hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mwenyekiti wa Bodi yabi Bima na Wajumbe wa Bodi hiyo, Viongozi wa Kampuni za Bima pamoja na Viongozi wa vyama miamvuli.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA.