Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA (TIRA) WALITEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA MAENDELEO YA BIMA YA INDIA (IRDAI)
03 Apr, 2024
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA (TIRA) WALITEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA MAENDELEO YA BIMA YA INDIA (IRDAI)

Machi 5, 2024 ujumbe kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania -TIRA umetembelea Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi na Maendeleo ya Bima ya India - IRDAI na kufanya mazungumzo ya kikazi na Menejimenti ya Mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Debashish Panda.

Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine IRDAI walieleza uzoefu wao katika kusimamia bima za kilimo na Afya ambapo wamesema tangu kuanza kwa skimu za bima ya kilimo tayari wameshalipa fidia ya majanga mbalimbali ya mazao yenye thamani ya USD B 14.

Kwa upande wake Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware  amesema ziara hiyo ni ya muhimu hasa ikizingatiwa India imepiga hatua kubwa kwenye usimamizi na matumizi ya Bima ya Afya na kwa vile Tanzania tunaanza utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote.

Kwa upande wake Mkt. wa Bodi ya Taifa ya Bima CPA Moremi Marwa ameishukuru IRDAI kwa ushirikiano na kusema kuwa uzoefu uliopatikana kwenye ziara hiyo utasaidia kuimarisha utendaji wa TIRA.
Viongozi wote wa pande mbili wamekubaliana kushirikiana na kubadilishana taarifa za masuala ya bima.