Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Shirikianeni na Tira Kukinga Wananchi Dhidi ya Majanga.
16 Sep, 2022
Shirikianeni na Tira Kukinga Wananchi Dhidi ya Majanga.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga amewataka Makatibu wakuu nchini kuhakikisha wananchi wanakingwa na huduma za bima. 

Balozi Kattanga ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo maalum ya umuhimu wa sekta ya bima katika shughuli za kijamii na kiuchumi nchini.

“Shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zinazoendelea nchini zinahitaji sekta ya bima iliyoimara ili kuhakikisha maendeleo yetu ya kiuchumi yanalindwa” Balozi Kattanga.

Amesema kwa kuwa masuala ya bima ni mtambuka na yanagusa Wizara/Taasisi mbalimbali ni vema yakashughulikiwa kwa pamoja badala ya kuiachia Wizara au Taasisi moja tu.

Ninaamini mabadiliko haya ya sheria yataendeleza ukuajia wa soko letu la bima kwani pamoja na takwimu za miaka sita kuonyesha kuwa soko letu linakuwa kwa wastani wa asilimia 7% bado ukuaji huu hauendani na mchango wa sekta hii muhimu katika pato la taifa; Hivyo ni muhimu mfahamu maana ya Sheria hii ya Bima ya lazima Kattanga.

Pia, amewakumbusha kuwa serikali imedhamiria kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kuboresha na kuinua uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja. Hivyo, unahitajika ushirikiano ili kuhakikisha shughuli zote za kiuchumi na kijamii zinakingwa na sekta hii ya Bima.

“Tuwape ushirikiano TIRA ili waweze kutekeleza sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009 na Sheria ya Fedha namba 5 ya mwaka 2022 inayoelekeza kuwepo kwa bima za lazima (mandatory insurance) kwa kujumuisha bima za masoko ya umma, majengo ya biashara, bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje, vyombo vya baharini na vivuko” alisisitiza Balozi.  Kattanga.