Nane Nane Arusha: TIRA na utoaji elimu ya bima, makundi mbalimbali yanufaika

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia kanda ya Kaskazini Arusha inashiriki Maonesho ya Wakulima jijini humo katika viwanja vya Nane Nane Njiro yaliyoanza tarehe 1 Agosti na kutarajiwa kumalizika Agosti 8, 2025. Lengo la ushiriki huo ni kutoa elimu ya bima lakini pia kusikiliza maoni mbalimbali ya wananchi.
Aidha, leo Agosti 3, 2025, banda la TIRA limetembelewa na wanafunzi mbalimbali kutoka Young Boys Academy ambao wamepewa elimu ya bima kwa kuelezwa umuhimu wa bima mbalimbali ikiwemo bima za afya na kuaswa kuwa mabalozi wazuri wa bima kwa wengine ili kukuza kizazi kinachofahamu umuhimu wa kuwa na kinga dhidi ya majanga.
Kwa upande mwingine, elimu kuhusu bima ya kilimo, uvuvi na ufugaji inaendelea kutolewa katika maonesho hayo kwa ajili ya kuhamasisha kukinga mali dhidi ya majanga kama ukame, mafuriko na wadudu waharibifu.
#Kaributukuhudumie
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA