Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha atembelea banda la TIRA Saba Saba na kupongeza “Kijiji cha Bima” katika utoaji elimu

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa C. Omolo Julai 04, 2025 alitembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika Maonesho ya Saba Saba na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya katika kukuza sekta ya bima lakini pia alitoa pongezi kwa uwepo wa Kijiji cha Bima kilichokusanya watoa huduma za bima mbalimbali katika maonesho hayo.
Bi. Omolo alielezwa ushiriki wa Mamlaka katika Maonesho hayo ya 49 ya Kimataifa ya Biashara; Saba Saba, ulioshirikisha watoa huduma za bima zaidi ya thelathini wakiwemo kampuni za bima na benki wakala wa bima, lakini pia uwepo wa darasa maalumu katika maonesho hayo maalum kwa ajili ya kutoa semina kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Aidha, Bi. Omolo alielezwa kuhusu vipaumbele mbalimbali vya Mamlaka kama Usimamizi wa skimu za Bima ya Afya.
Mbali na TIRA pia alitembelea baadhi ya mabanda kufahamu zaidi kuhusu huduma zitolewazo.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA