Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Naibu Kamishna apongeza ushiriki wa kampuni za bima Wiki ya Huduma za Fedha, atoa Rai ya kuimarisha utoaji elimu
22 Jan, 2026
Naibu Kamishna apongeza ushiriki wa kampuni za bima Wiki ya Huduma za Fedha, atoa Rai ya kuimarisha utoaji elimu

Naibu Kamishna Bi. Khadija Said ametoa pongezi hizo kwa kampuni za bima kwa ushiriki wao  katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea viwanja vya Usagara Tanga, amesema mchango wao ni muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za bima na ulinzi wa kifedha.

Akizungumza wakati wa ziara katika mabanda ya kampuni hizo, Naibu Kamishna amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya bima kwa makundi yote ya jamii, hususan vijana na wafanyabiashara wadogo, ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kujikinga dhidi ya vihatarishi mbalimbali na pia ametoa msisitizo zaidi juu ya uelimishaji kuhusu bima ya afya kwa wote.

Kampuni zilizoshiriki ni pamoja NIC, ZIC, Bumaco, Meticulous Gen. Insurance, Sanlam Allianz,MO Assurance, Britam Insurance na kampuni ya bima mtawanyo ya Grand Re.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA