Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa asisitiza utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote
06 Jul, 2025

Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa CPA Moremi Marwa ametoa msisitizo huo wa Utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) katika Maonesho ya Saba Saba hapo jana Julai 4,2025.
Mwenyekiti huyo wa Bodi pia alisisitiza juu ya uelimishwaji zaidi kwa wananchi kuhusu Bima ya Afya kwa wote na kuipongeza TIRA kwa kuwa na "Kijiji cha Bima" katika Maonesho hayo ambacho kimeleta kwa pamoja kampuni za bima, mawakala wa Bima na hata Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF).
Aidha, aliongeza Bima ya Afya kwa wote itawasaidia wananchi kutokusumbuka na matibabu na hatimae kufanikisha maono ya Taasisi na Serikali yetu kwa ujumla katika mafanikio zaidi eneo la afya.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA