Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Maonesho ya Nane Nane : Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, atembelea mabanda yanayoiwakilisha Sekta ya Bima kwenye kilimo
07 Aug, 2025
Maonesho ya Nane Nane : Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, atembelea mabanda yanayoiwakilisha Sekta ya Bima kwenye kilimo

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama, Bi. Happyness John Sule, atembelea mabanda yanayoiwakilisha Sekta ya Bima kwenye kilimo yakiwemo banda la TIRA, TAIC na TIO katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane Dodoma.

Akiwa kwenye ziara hiyo, Bi. Sule amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za utoaji wa elimu ya bima kwa wananchi, ili kuongeza uelewa na kuwahamasisha kuitumia bima kama nyenzo ya maendeleo.

Ameeleza kuwa Wilaya ya Mkalama iko tayari kupokea elimu hiyo ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma za bima, sambamba na kuzitumia kama kichocheo cha fursa za kiuchumi na kijamii.