Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Aridhini – TIRA tunashiriki
Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Aridhini – TIRA tunashiriki
Ni jijini Dar es Salaam katika viwanja vya kihistoria vya Mnazi Mmoja ambapo yanaendelea Maadhimisho ya Kwanza ya Wiki ya Usafiri endelevu ardhini, TIRA tunashiriki kwa lengo la kutoa elimu ya bima ikiwemo bima ya vyombo vya Moto. Maadhimisho hayo yameanza rasmi Novemba 24 – 29, 2025 na yameandaliwa na LATRA.
Aidha, akifungua rasmi Maadhimisho hayo Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Mwakiposa Kihenzile katika hotuba yake amesema lengo ni kuelimisha wananchi kuhusu shughuli za usafirishaji unaotunza mazingira kama umeme na gesi na kutoa wito kwa wananchi kushiriki katika mabanda mbalimbali ili kuelimika kuhusu masuala ya usafirishaji.
TIRA na LATRA ni wadau muhimu katika sekta ya usafirishaji ambapo pia wapo katika hatua muhimu ya kuwezesha upatikanaji wa tiketi za vyombo vya usafiri za kielektroniki (e – ticket) ambazo zitatoa taarifa muhimu kwa msafiri kuhusu mtoa huduma za bima wa Chombo husika, hatua itakayomsaidia msafiri kufatilia madai ya bima endapo janga lolote litatokea.
TIRA tunakukaribisha viwanja vya Mnazi Mmoja kwa huduma mbalimbali za bima.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA.
