Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kazi na Afya: Watumishi TIRA wakutana pamoja, washiriki michezo mbalimbali 
21 Aug, 2025
Kazi na Afya: Watumishi TIRA wakutana pamoja, washiriki michezo mbalimbali 

Mkoani Pwani wilayani Bagamoyo katika eneo lenye mandhari ya kuvutia na utulivu, lililozungukwa na miti na vichaka, ndipo watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) walipokutana na kufurahia tukio lililoacha kumbukumbu ya kipekee. Tarehe 20 Agosti 2025, walitembelea eneo la Ndoto Polepole kushiriki michezo ya kujenga mwili na akili sambamba na kuimarisha mshikamano wao wa kikazi.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na uongozi wa juu, menejimenti pamoja na watumishi wa TIRA kutoka maeneo mbalimbali nchini. Kupitia michezo ya kutumia utashi, lengo lilikuwa kuongeza mshirikiano na kuboresha utendaji kazi. Aidha, michezo ya kufurahisha kama kuvuta kamba, kuendesha baiskeli na karata ilifanyika. Wafanyakazi wenye vipaji vya uchoraji, uimbaji na kucheza muziki nao walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao, ikilenga kuburudisha na kuonesha mshikamanano wa pamoja nje ya mazingira ya kazi.

Shughuli hizi zilifanyika mara baada ya Kikao cha Wafanyakazi 2025 kilichoandaliwa na Kurugenzi ya Utawala na Rasilimali Watu tarehe 19 Agosti 2025. Katika Kikao hicho, semina mbalimbali kuhusu uboreshaji wa ufanisi kazini na afya ya akili ziliendeshwa, kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi watumishi na kuongeza tija katika kuimarisha utendaji kazi wa taasisi hiyo.

TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA