Kanda ya Ziwa Tanganyika pamoja na wadau sekta ya bima washiriki kikamilifu kampeni ya kijani
Watumishi wa Kanda ya Ziwa Tanganyika kwa kushirikiana na Wadau wa Bima kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kampuni la Bima la Milembe, NBC-Benki Wakala na Makampuni ya Bima ya Triple G na Jovin wameshiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika kwenye Kiwanja cha Ofisi cha TIRA kilichopo Mtaa wa Ilembo, Mpanda katika Mkoa wa Katavi.
Akieleza zaid Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa Tanganyika Bw. Ahaz Joel amesema zoezi hilo limefanyika leo tarehe 27Januari, 2026 ikiwa ni kuunga mkono Kampeni ya Kijani ya kitaifa sambamba na kumtakia heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa vitendo Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi hao pamoja na Wadau wa Bima walishiriki katika zoezi hilo muhimu kwa utunzaji wa mazingira, wamesisitizwa kujenga Utamaduni wa kutunza mazingira pamoja na kupanda miti.
