Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kamishna wa Bima atembelea Kijiji cha bima; apongeza maandalizi na ushiriki wa wadau
08 Jul, 2025
Kamishna wa Bima atembelea Kijiji cha bima; apongeza maandalizi na ushiriki wa wadau

Kilele cha Maonesho ya Saba Saba hapo jana Julai 7, 2025 “Kijiji cha Bima” kilitembelewa na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware, ambaye alitembelea mabanda ya watoa huduma za bima wakiwemo kampuni za bima, benki wakala wa bima na kampuni za bima za Takaful na kuelezwa kuhusu huduma mbalimbali wazitoazo ndani ya maonesho hayo. Lakini pia kupongeza ushiriki wao na kamati ya maandalizi kwa kazi nzuri.

Dkt. Saqware pia alitembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima TIRA na kupewa taarifa mbalimbali tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 28, 2025 na pia alitembelea banda la Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO).

Kijiji cha Bima kilizinduliwa rasmi Julai 4, 2025 na watendaji wakuu mbalimbali kutoka kwa kampuni za bima.

#Bima ya afya kwa wote, Fahari ya watanzania