Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kamishna wa Bima ana kwa ana na Mawakala wa Bima Tanzania - - wajadili masuala mbalimbali ya kisekta
29 Dec, 2025
Kamishna wa Bima ana kwa ana na Mawakala wa Bima Tanzania - - wajadili masuala mbalimbali ya kisekta

Leo Desemba 29, 2025 Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware amekutana na Mawakala wa Bima Tanzania lengo likiwa ni kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu maswala mbalimbali yanayowahusu watoa huduma hao wa bima.
Wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho Dkt. Saqware amesema Mawakala wa bima kwa sasa wanafikia 1473 ambapo ni sawa na 50% ya watoa huduma wote ambao jumla ni 2918 hivyo ni kundi muhimu kwenye sekta kwakuwa wanawafikia wananchi wengi zaidi. Kikao kazi hicho kimepokea pia maoni ya Mawakala na ushauri uliotolewa ili kuboresha utendaji wa huduma za mawakala na hatimae kufikia dhamira ya Serikali ya upatikanaji na usambazaji wa huduma za bima nchini.
Miongoni mwa hoja zilizotolewa mrejesho ni pamoja na mifumo ya kigitali na kamisheni. Kikao kazi hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi waandamizi wa TIRA, viongozi wa Mawakala wa Bima, Afande Deus Sokoni -Mrakibu Mwandamizi wa Polisi na Mawakala.