Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Kamishna wa Bima Dk. Baghayo A.Saqware amekutana na Menejiment ya OR-TAMISEMI
27 Jul, 2023
Kamishna wa Bima Dk.  Baghayo A.Saqware amekutana na Menejiment ya OR-TAMISEMI

Kamishna wa Bima Dk.  Baghayo A.Saqware amekutana na Menejiment ya OR-TAMISEMI ambapo ametoa uelewa kuhusu umuhimu wa huduma za Bima  na maeneo ya kushirikiana na kutoa wito kwa Uongozi wa TAMISEMI kuzingatia Sheria ya Bima Sura 394.

Kwa upande wa Menejimenti ya TAMISEMI ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Wilson Mahela amemshukru Kamishna kwa kuleta elimu ya Bima Wizarani na kuahidi kutoa ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali yanahusu bima kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 27 Julai katika ukumbi wa TAMISEMI- Dodoma. Kamishna aliambatana na Mkurugenzi wa Mipango,Utafiti na Masoko Ndg.S.Mwiru, Meneja wa Maendeleo ya Masoko Ndg Edgar na Meneja wa TEHAMA Ndg. Ali Othuman.