Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Huduma za bima kwa Watanzania ziendelee kutolewa kwa ubora zaidi - Mhe. Zena Said
11 Oct, 2025
Huduma za bima kwa Watanzania ziendelee kutolewa kwa ubora zaidi - Mhe. Zena Said

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mhandisi  Zena Ahmed Said, ameitaka sekta ya bima nchini kuwa wabunifu katika kuanzisha bidhaa mpya zitakazosaidia serikali kufikia lengo la kuchangia asilimia 3 ya Pato la Taifa ifikapo 2030.

Akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 yenye kaulimbiu “TIRA kwa Soko Salama la Bima”, Mhe. Zena alisema kampuni za bima zinapaswa kuboresha huduma, mazingira ya kazi na uwazi katika utoaji wa haki.

“Tujitahidi kufanya inavyotakiwa na kutumia mbinu za haraka kutatua changamoto. Ubunifu kama bima ya ndoa ni mfano wa mwelekeo tunaoutaka,” alisema.

Nae Naibu Kamishna wa TIRA, Bi. Khadija I. Said , alisisitiza umuhimu wa huduma bora na lugha yenye staha kwa wateja, akisema Serikali inaendelea kuimarisha sekta hiyo kupitia bidhaa mpya zenye manufaa kijamii.

Kwa upande wake Meneja wa TIRA Kanda ya Zanzibar, Bw. Kurenje Mbura, alisema vituo 103 vya mauzo ya bima vimesajiliwa visiwani na kwamba TIRA inakamilisha mfumo utakaojumuisha bima katika masharti ya kupata kadi ya kutembea barabarani.

Meneja wa Viwango, Bw. Frank Fred Shangali alimalizia kwa kuhimiza kampuni za bima kuzingatia viwango vya ubora na mifumo imara ya mawasiliano ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wateja.