Dkt Saqware: Vijana mna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko sekta ya bima kupitia ubunifu

Mei 24, 2025
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware ameyasema hayo wakati akitoa hotuba yake kwa wadau walioshiriki Bima Debate iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa chuo cha ACISP Masaki. Dkt. Saqware amesisitiza umuhimu wa vijana; wanafunzi wa sekondari na wanavyuo wasomi wabobezi masuala ya bima kuangalia changamoto mbalimbali katika soko na kuwa wabunifu kutatua.
Dkt. Saqware pia alisisitiza Mamlaka imechukua hatua mbalimbali kukuza ukuaji wa soko la bima nchini ambapo kwa miaka mitano (5) mfululizo soko linakua kwa asilimia 15% kila mwaka hii ikiangazia viashiria mbalimbali kama ongezeko la watoa huduma wa bima, ongezeko la ajira katika sekta, ubakizwaji wa ada ya bima nchini na mambo mengine mbalimbali.
Kamishna pia alizipongeza shule na vyuo vilivyoshiriki, majaji na waandaaji wa Bima Debate kufanikisha tukio hilo muhimu katika kukuza uelewa wa bima nchini. Bima Debate imefanyika kuelekea Siku ya Bima kitaifa (Insurance Day 2025) na iliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) kwa kushirikiana na TIRA.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA