Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa CPA Moremi Andrea Marwa afungua kikao cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA)
31 Aug, 2023
Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa CPA Moremi Andrea Marwa afungua kikao cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA)

Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa CPA Moremi Andrea Marwa amefungua rasmi kikao kazi cha wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) leo tarehe 30 Agosti 2023, Mkoani Tanga.
Akihutubia wafanyakazi hao  CP A Moremi Andrea Marwa amesisitiza ubunifu katika ufanyaji kazi ili kuleta Imani na tija kwa wadau wa sekta ya bima. 
Kwa upande wake Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware alisema kuwa kwenye mkutano huo watumishi wanajadili, kutafakari changamoto na kuweka mikakati mbalimbali kwa pamoja ya kuhakikisha Mamlaka inaongeza tija kwenye Soko la Bima. 
Huu ni utaratibu ambao Mamlaka umejiwekea wa watumishi wake kukutana kila mwaka kwa ajili ya kikao kazi ambapo kwa mwaka huu ni kikao cha Pili.