Bima Debate mtanange wa kielimu kukuza uelewa wa bima nchini

Mei 24, 2025
Bima Debate inaendelea hapa katika ukumbi wa chuo cha ACISP ambapo shule mbalimbali za Sekondari kutoka mkoa wa Dar es Salaam zimekutana kujadiliana na kutoa maoni kuhusu mada mbalimbali ikiwemo inayosema Je Bima inasaidia kukuza uchumi wa Tanzania? Lakini pia mada inayohusu umuhimu wa bima ya afya kwa jamii. Mgeni Rasmi akiwa ni Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware.
Aidha, Bima Debate hii ni sehemu ya kionjo kuelekea Siku ya Kitaifa ya Bima (Insurance Day) itakayofanyika June 18 -21 jijini Arusha na imeandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Shule zinazoshiriki Bima Debate ni pamoja na Shule ya Sekondari Jangwani, Zanaki, Midland, Shaaban Robert na Kisutu Sekondari. Bima Debate hii ni sehemu ya mikakati ya sekta ya bima katika kukuza uelewa wa masuala ya bima nchini ambapo pia ni muhimu kuanzia kwa watoto na vijana ambao ni taifa la kesho.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA