Ufanisi wa Huduma za Bima kwa Wananchi; Kamishna afanya ziara kanda kumi za Mamlaka
Na. Abubakari Kafumba
Katika kuzingatia ufanisi na huduma bora zaidi zinatolewa kwa wananchi Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware anaendelea na ziara maalum ya kutembelea kanda kumi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) zilizopo nchi nzima. Ziara hiyo imeanza rasmi Novemba 9 2025 katika Kanda ya Kusini na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo likiwa kufanya tathmini ya utendaji kazi wa kanda hizo na kiwango cha huduma za bima zipatikanazo katika mikoa hiyo ili kuhakikisha huduma ya bima inamfikia kila mwananchi.
Hapo jana Novemba 13, 2025 Kamishna pamoja na viongozi wengine wa Mamlaka walitembelea Kanda ya Ziwa Tanganyika inayohudumu mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma mbali na Kikao kilicholenga tathmini ya huduma za bima ikiwemo utekelezaji wa mpango wa bima ya afya kwa wote, pia uongozi huo ulitembelea eneo maalumu ambalo litajengwa ofisi za Kanda hiyo.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA
