Mafunzo Ya Mabalozi Wa Bima Nchini
Mamlaka ya Uisimamizi wa Bima Nchini (TIRA) kwa kushirikiana na wadau wa bima imefanikiwa kuwapata mabalozi watatu wa kitaifa wa bima ambao pamoja na majukumu yao watasaidia kutoa elimu na uelewa wa bima kwa umma. Aidha mabalozi watakuwa na jukumu la kuishauri Mamlaka kwa lengo la kukuza na kuendeleza sekta ya bima nchini. Pichani ni mabalozi hao wa bima wakipokea vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo ya mda mfupi ya bima, majukumu yao na udhibiti wa vihatarishi. Mafunzo hayo yametolewa na London School of Insurance nchini Uingereza.
Mabalozi wa kitaifa wa bima pichani kutoka kushoto ni Mhe. Mhandisi Zena Said (Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar), Mhe. Wanu Hafidh (Mbunge), na Mhe. Japhet Hassunga (Mbunge). TIRA Kwa Soko Salama la Bima.
Pichani Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Said akimkabidhi Mhe.Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. AshaRose Migiro taarifa za mafanikio na maendeleo ya soko la Bima, ikiwa ni pamoja na miongozo mbalimbali ya bima. Mhe Mhandisi Zena yuko nchini Uingereza kwenye mafunzo ya mabolozi wa bima nchini. Mafunzo hayo yalianza tarehe 23 hadi 27 Machi 2023 katika London School of Insurance nchini Uingereza. Hongereni sana wadau wa soko la bima.