Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Chakechake yanufaika na elimu ya bima - wadau wapata nafasi kutoa maoni yao
25 Feb, 2025
Chakechake yanufaika na elimu ya bima - wadau wapata nafasi kutoa maoni yao

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Rashid Hadid Rashid amezitaka taasisi za bima kuwa na ushirikiano na jamii katika kutatua kero zinazowakabili ili kuimarisha huduma za bima nchini.

Wito huo umetolewa Kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Mkoani Hamad Omar Bakar katika mkutano wa kupokea maoni juu ya kuboresha huduma za Mamlaka ya Bima (TIRA) nchini.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema ili  huduma za bima ziweze kuwa bora na kuleta ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii ni muhimu kukaa na wadau wake kuona changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi wa kina.

Mapema Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Bima Bi. Khadija Issa Said amewataka wadau kuwa huru katika kutoa maoni yao katika kuboresha huduma za Mamlaka hiyo ili kuhakikisha inatoa huduma stahiki na Kwa ufanisi Kwa jamii.

Nao baadhi ya wadau hao wameiomba Mamlaka ya Bima kuwa na majibu ya kutosholeza pale mdau anapopata tatizo kutokana na kuchelewa Kwa muda mrefu wa  kulipwa fidia Kwa mdau , huku wakiiomba TIRA kuchukua juhudi za makusudi kutoa elimu juu ya umuhimu wa bima Kwa jamii.

TIRA, KWA SOKO SALAMA LA BIMA.