The United Republic of Tanzania

Tanzania Insurance Regulatory Authority

“TIRA kwa Soko Salama la Bima”
TIRA NA ARIS WAANZA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO; KAMISHNA WA BIMA ASHIRIKI
07 Nov, 2026
TIRA NA ARIS WAANZA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO; KAMISHNA WA BIMA ASHIRIKI

Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, leo Novemba 6, 2026 ameshiriki hafla fupi ya kuwaaga mashujaa 22 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na kampuni ya ushauri wa bima ya ARIS  ambao wameanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Geti la Machame.

Safari hiyo ni sehemu ya maadhimisho kuelekea Miaka 30 ya utoaji huduma za bima ya kampuni ya Ushauri ya ARIS ambapo inalenga kupaza sauti juu ya umuhimu na matumizi ya bima nchini.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Saqware ambae ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo amesema tukio hilo ni moja ya hatua ya utekelezaji wa Dira 2050, ambayo pia inasisitiza ushirikiano wa taasisi za umma na binafsi katika kuleta maendeleo kwa taifa.

"ARIS wameonesha dhamira ya kueneza elimu ya bima kupitia kupanda mlima Kilimanjaro. Na sisi kama TIRA, tumeona ni jambo jema na hivyo kushirikiana nao katika tukio hili muhimu," amesema Dkt. Saqware

Ameongeza kuwa kupitia tukio hilo ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii nchini, hasusan Mlima Kilimanjaro, na pia ni fursa ya kutangaza kimkakati shughuli za bima ambazo TIRA inazisimamia.Wapanda mlima wamekabidhiwa bendera zinazotarajiwa kupeperushwa katika Kilele cha mlima Kilimanjaro kama ishara ya kwamba elimu ya bima inapaswa kufika mbali kabisa ili Watanzania wote wapate kuifahamu na hatimaye kutumia huduma hizo muhimu.