The United Republic of Tanzania

Tanzania Insurance Regulatory Authority

“TIRA kwa Soko Salama la Bima”
Menejimenti ya TIRA yanolewa mafunzo ya uongozi na utoaji wa huduma bora
30 Oct, 2026
Menejimenti ya TIRA yanolewa  mafunzo ya uongozi na utoaji wa huduma bora


Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Events Maestro Africa, imeendesha mafunzo kwa Wakurugenzi na Mameneja wa Idara mbalimbali za TIRA kuhusu Uongozi Bora, Huduma Bora na Maisha Bora. Mafunzo hayo yamefanyika TIRA Bima House, Njedengwa, Dodoma, Oktoba 29, 2026.


Akiongoza mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Events Maestro Africa, Dkt. Tatu-Maureen Mnimbo, amewahimiza viongozi kuwa mfano bora kwa wafanyakazi wao, kuboresha huduma na kuzingatia misingi ya maisha bora.


Akihitimisha mafunzo hayo, Naibu Kamishna wa Bima, Bi. Khadija Issa Said, ameishukuru Events Maestro Africa na kusisitiza umuhimu wa viongozi kushirikiana na wafanyakazi, kuwajengea uwezo na kutatua changamoto zinazojitokeza kazini.