Huduma Bora kwa Wananchi: TIRA yashiriki Uzinduzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Mtumba Dodoma
30 Oct, 2026
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, iliyofanyika leo, tarehe 30 Oktoba 2026. Hafla hiyo imeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
