Watumishi TIRA wapewa mafunzo ya Afya ya akili na Maadili katika Utumishi wa Umma

Watumishi TIRA wapewa mafunzo ya Afya ya akili na Maadili katika Utumishi wa Umma
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware amefungua rasmi mafunzo ya siku moja kwa watumishi wa Mamlaka hiyo yahusuyo Afya na Rushwa, leo Februari 1, 2025 katika ukumbi wa TAGLA ndani ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Mafunzo hayo yana lengo la kuwanoa katika maeneo hayo muhimu.
“Mafunzo haya ni muhimu kwa ustawi wenu, wanaowategemea, taasisi na Serikali yetu kwa ujumla’ amesema Dkt. Saqware, ambapo amewataka watumishi kulinda afya zao na kujikinga na vitendo vya kutoa rushwa katika kulinda utumishi wao na ustawi wa serikali.
Katika mada ya Afya ya Akili, watumishi walipewa elimu hiyo na namna ya kuishi kuepuka msongo wa mawazo hasa mahali pa kazi na kujikinga na tabia hatarishi kama ulevi, uvutaji bangi na vitendo vya ngono uzembe.
Lakini pia katika mada ya pili ya Maadili, watumishi walikumbushwa kanuni nane (8) za Maadili katika utumishi wa Umma zikiwemo kutoa huduma, utii kwa Serikali, Bidii ya Kazi, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu na nyinginezo. Ili kufanya kazi kwa bidii na ueledi.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA