Wanawake TIRA washiriki kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake jijini Arusha
11 Mar, 2025

Leo tarehe 8 machi 2025 Wanawake TIRA wakiongozwa na Naibu Kamishna wa Bima Tanzania Bi. Khadija Said wameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alikuwa Mgeni Rasmi.
Akisoma hotuba yake Rais Samia amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa hatua hiyo imedhihirisha wao sio tu jeshi kubwa bali ni jeshi madhubuti na la kuaminiwa.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa maonesho yaliyofanyika kwa wiki moja ambapo TIRA ilishiriki katika utoaji wa elimu ya bima kwa wananchi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kibima.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA